HALMASHAURI 95 ZAPATA MAGARI KUPITIA PROGRAMU YA EP4R
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amekabidhi magari 25 ikiwa ni sehemu ya Magari 200 yaliyoagizwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kwa ajili ya Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri zote nchini. Pia ameahidi kujenga bweni la wanafunzi wa kiume wa shule ya sekondari Kibasila ikiwa ni ahadi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan. Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika hafla ya ugawaji wa magari hayo Mhe. Kairuki aliwataka Wakala wa Ununuzi Serikalini (GPSA) kukakamilisha upatikanaji wa magari mengine 105 yaliyosalia kwa ajili ya mafisa elimu hao. "Katika Halmashauri 184 zinazotakiwa kupata magari, Halmashauri 51 tayari zimepata katika awamu ya kwanza, awamu ya pili 19 na hii awamu ya tatu magari 25 hivyo bado magari 105 kwa maofisa hayo," alisema. Aidha, ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha elimu na maslahi ya walimu nchini hivyo aliwataka maofisa hao wa...