HALMASHAURI YA GEITA MJI YAFANYA ZIARA CHALINZE DC
Halmashauri ya Geita mji hii leo imefanya ziara katika Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani kwa lengo la kutembelea na kujifunza namna bora ya uzalishaji na utekelezaji wa madini ujenzi.
Ugeni huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mh. Cornel Magembe Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Costantine Mtani ,Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zahara Michuzi,Waheshimiwa madiwani,Wataalamu na Baadhi ya wananchi wakiwa wawakilishi wa Wananchi wenzao.
Kwa niaba ya Halmashauri ya Geita MJI,Mkuu wa Wilaya huyo Pamoja na Mwenyekiti wameshukuru Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa Mapokezi mazuri lakini pia kwa kuwapa maelekezo mazuri ya namna bora ya uzalishaji wa miradi.
''Tunawashukuru sana kwa mapokezi mazuri sana pamoja na namna mlivyotupa maelekezo mazuri kwani hamkutuficha kitu lakini pia huu ni mwanzo tutaendelea kujifunza zaidi na zaidi kwani sasa ni kitu kimoja '' Amesema Mh.Magembe
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mhe: Hassani Mwinyikondo kwaniba ya Halmashauri yake amewashukuru Wageni hao kuja kujifunza katika Halmashauri ya Wilaya Chalinze lakini pia Chalinze imejifunza mengi kwa ujio wao.
Aidh Mhe: Hassani Mwinyikondo amewaahidi wageni hao kuwa nao wategemee Halmashauri ya Chalinze kufanya safari ya kwenda kujifunza zaidi katika Halmashauri ya Geita Mji.
Ugeni huo ulipata wasaa wa kutembelea eneo la Makarasha yanayotumika kuzalisha kokoto lakini pia kuona vizuia vikubwa vya kukatia ushauru wa kokoto vilivyofungwa kamera kwa ajili ya kuzuia utoroshaji wa mapato pamoja na kutembelea kituo kipya cha Radio cha Chalinze FM.


Comments
Post a Comment