RC KUNENGE AFANYA ZIARA HOSPITALI YA WILAYA MSOGA


Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge hii leo ameanya ziara maalumu katika hospital ya Msoga kwa lengo la kukagua na kuona maendeleo ya Jengo la dhararu la (EMD) Iliyopo katika hospital ya Msoga .


Akiwa katika hospitali hiyo Mhe Kunenge alipata kuona maendelea ujenzi wa jengo la hilo la dharura ambalo ujenzi huo umekamilia kwa asimilia kubwa na kilichobaki ni umalizaji wa uwekezaji wa samani,Ujenzi wa majengo mbalimbali katika hospitali hiyo Pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa uwanja wa kisasa wa Mpira wa miguu.


Katika ziara hiyo Mhe Kunenge alipata wasaa wa kusalimiana na kuzungumza na wananchi waliofika katika hospitali ya Msoga kupata huduma ambapo alisema alitembelea hospitali hiyo kuona maendeleo ya ujenzi lakini pia kuona namna huduma  zinazotolewa hospitalini hapo.


''Nimekuja kuona Maendeleo ya ujenzi wa jengo ya huduma za dharura lakini pia kuona jinsi utoaji wa huduma unavyoendelea na naamini ninyi ndiyo mtawaambia huduma ina ubora ama sivyo”.Amesema Mhe.Kunenge


Aliendelea kwa kusema kuwa,kukamilika kwa jengo la huduma za dharura Kutasaidia hduma mbalimbali ambazo zinapatikana hospitali ya Muhimbili ziweze kupatikana katika hospitali hiyo.


Aidha Mhe Kunenge amewaambia wananchi hao kuendelea Kumuombea kwa Mungu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani ili awe na afya njema ili kuweza kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea miradi mbalimbali Lakini pia kuendelea kuwajengea zahanati katika maeneo mbalimbali ili kuwapunguzia umbali.


Mzee Juma Omary alizungumza kwa niaba ya wananchi waliokuwa katika hospitali hiyo alitoa pongezi kwa Raisi wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo yao.


“Tunamshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na chama cha mapinduzi kwa jitihada madhubuti zinazosababisha sisi wananchi wa chini kupata huduma za afya kwa wakati zenye uhakika lakini pia zimesababisha wananchi tumeweza kupata huduma katika maeneo yetu ya karibu."Amesema Mzee.Ally.




Comments

Popular posts from this blog

DC-OKASH,KAMATI YA USALAMA WAFANYA ZIARA VIWANDANI CHALINZE

TAASISI YA BLUE CARBON UAE NA SERIKALI YA TANZANIA WAMETIA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO