CHALINZE DC FC YAANZA MAANDALIZI YA SHIMISEMITA 2023
Timu ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeanza kujiandaa na mashindano ya SHIMISEMITA kwa kucheza mechi mbalimbali za kirafiki ikiwemo mechi ya leo ambapo timu ya Chalinze Dc imepoteza kwa magoli 8-4 dhidi ya Azam Veterani katika uwanja wa Azam Compex,Chamanzi.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa kirafiki Mbaraka Shabani (Cantona)ambaye ni Mwenyekiti wa Timu ya Azam Veterani amesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa Chalinze DC FC kwani mpaka hivi sasa pande mbili hizo zimekuwa kama ndugu.
" Nimefurahishwa na ugeni wenu kwani sasa tumekuwa kama ndugu naamini mmejifunza mengi lakini pia hata sisi tumejifunza mengi sana kwani mpira mnaujua na najua hamkutarajia kutowakuta veterani wenyewe hii ni kutokana na Timu yetu ya Azam Fc kusafiri kwenda Dodoma na viongozi ambao ndio wachezaji wetu hivyo basi niwakaribishe tena siku nyingine kwani mechi hizi za kirafiki zinatuandaa vyema kiafya na hata kimichezo".Amesema Ndg.Mbaraka Shabani.
Aidha uongozi wa Klabu hiyo umemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndg. Ramadhani Possi kwa kuhakikisha timu ya Chalinze DC inashirikiana vyema na timu ya Azam Veterani na kuahidi kufika katika Ofisi za Halmashauri na kuonana nae ili waweze kuanzisha mashirikiano mazuri zaidi katika michezo.
Nae Afisa Habari Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndg.Sama Lucian ameushukuru uongozi wa Azam kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi hizi mbili kwa upande wa Serikali na taasisi binafsi.
"Kwanza kwaniaba ya Viongozi wa Halmashauri nitoe shukrani zangu za dhati kwa ukaribisho mzuri katika Taasisi hii ya Azam tumefurahishwa na mapokezi yao mazuri sisi tuahidi tu tutaendelea kuwa karibu siku zote na kudumisha ushirikiano zaidi na pia tunawakaribisha sana Halmashauri ya Chalinze kuja kututembelea muda wowote.Amesema Ndg. Sama.
Nae Kocha Mkuu wa Kikosi cha Chalinze Dc FC Mwl.Julius Jeremiah amesema kuwa kwasasa timu ya Halmashauri itaendelea kupata mechi za kirafiki kwa wingi ili kujijenga zaidi na kuijengea uzoefu zaidi katika mashindano ya mbeleni hasa ya SHIMISEMITA kwani ndio lengo kubwa.

Comments
Post a Comment