DC-OKASH,KAMATI YA USALAMA WAFANYA ZIARA VIWANDANI CHALINZE
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Halima Okash pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama amefanya ziara katika maeneo ya uwekezaji na Viwanda vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani Pwani kwa lengo la kuona Mafanikio,uendeshaji na Changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili kuweza kuzitatua ili kuweka mazingira salama kwa wawekezaji.
Akizungumza katika Ziara hiyo Mhe.Okash amewapongeza wawekezaji hao kwa Uwekezaji Mkubwa wanoufanya katika Halmashauri ya Chalinze kwani ni manufaa kwa Halmashauri,Wilaya,Mkoa na hata Taifa kwa ujumla pamoja na jamii inayowazunguka pamoja na kuwaahidi kuzifanyia kazi changamoto wanazokumbana nazo ili kuendelea kuwawekea Mazingira rafiki katika Uwekezaji .
“Niwapongeze wawekezaji hasa kwa uwekezaji Mkubwa mnaoufanya kwani haya ni maendeleo makubwa kwa Taifa kwani Tanzania sasa tunaouwezo mkubwa wa kutumia bidhaa za ndani na kuzisafirisha mpaka nje ya nchi na niwaahidi sisi kama Serikali tutazifanyia kazi Changamoto zote ili muwe na Mazingira rafiki katika uzalishaji”.Amesema Mhe. Okash.
“Vilevile niwapongeze sana kwa Wawekezaji kwa jinsi mnavyojitoa kwa jamii kwa kurudisha shukrani kama vile katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa,Zahanati lakini pia utoaji wa ajira kwa vijana waishio katika Halmashauri hii ili kuwaongezea kipato na uwezo katika wa kazi.”Aliongeza.
Hata hivyo Mhe.Okash amewaomba wawekezaji hasa wa Kiwanda cha SAYONA kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ni aina gani ya matunda au malighafi zinazohitajika kwa wingi katika uzalishaji ili Ofisi hiyo iweke kipaumbele katika kutoa Mikopo ya asilimia 10 kwa Vijana ili waweze kuanza Shughuli za Kilimo za Matunda hayo ndani ya Halmashauri ya Chalinze.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndg.Ramadhani Possi ameendelea kuwataka Wawekezaji hao kuendelea kulipa kodi kwa wakati ili kuweza kuongeza mapato ndani ya Halmashauri na Serikalini pamoja na kuwapongeza kwa kujitoa kwao katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika Shughuli za maendeleo.
Ikumbukwe kuwa katika ziara hiyo Mhwshimiwa Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama imeweza kutembelea Viwanda mbalimbali vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ikiwemo Kiwanda cha kutengeneza juisi cha SAYONA,Kiwanda cha kutengeneza malumalu au vigae vya chini KEDA CERAMICS COMPANY LIMITED pamoja na Kiwanda cha utengenezaji wa Viroba cha H&J FACTORY.


Comments
Post a Comment