BARAZA LA MADIWANI CHALINZE LAPITISHA RASIMU YA BAJETI YA BILIONI 52.6 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024


BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze limepitisha rasimu ya bajeti  ya mwaka wa fedha 2023/2024 sh. Biln 52.6  itakayotekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo. 

Akiwasilisha makadirio hayo katika kikao cha Baraza la Bajeti Mkurugenzi Ramadhani Possi amesema kati ya fedha hizo sh. Biln 32.7 ni ruzuku kutoka Serikali kuu, Biln 14.9 Makusanyo ya ndani na sh.Biln 4.9 ni kutoka kwa wahisani.

Amesema feha hizo zitatumika kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, mishahara ya watumishi na matumizi ya ofisi.

Akizungu



mza katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassan Mwinyikondo pamoja na baadhi ya Madiwani wa waamepongeza bajeti hiyo na kuasema inakwenda kuwakomboa wananchi wa Chalinze.

Mwinyikondo amesema Maendeleo katika Halmashauri hiyo yanaenda kwa kasi kutokana na ushirikiano kati ya Madiwani na wataalamu.

" Katika makusanyo ya ndani kwa  mwaka wa fedha 2022/2023 tulikadiria sh Biln 13 na hadi sasa tumekusanya kwa asilimia 55 kwa bajeti hii inayoendelea, tunampongeza Rais kwa hali inayoonekana nchi inaenda vizuri na maendeleo yanapatikana" amesema Mwinyikondo. 

Akitoa Salamu za Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo Salum Gumbo alisema makadirio hayo ya bajeti endapo yatapitishwa yataenda kutatua vikwazo kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini.

Gumbo amesema Mkuu huyo wa Wilaya amewaomba Madiwani kufuatilia fedha zinazotengwa kwenye miradi iliyokusudiwa zitumike kama zilivyoelekezwa.

Aidha maelekezo pia yametolewa kwa watendaji kuanzia ngazi ya Kata kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji itatuliwe kwa wakati na kuruhusu shughuli za maendeleo kufanyika.


Comments

Popular posts from this blog

DC-OKASH,KAMATI YA USALAMA WAFANYA ZIARA VIWANDANI CHALINZE

TAASISI YA BLUE CARBON UAE NA SERIKALI YA TANZANIA WAMETIA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO

RC KUNENGE AFANYA ZIARA HOSPITALI YA WILAYA MSOGA