Posts

Showing posts from February, 2023

RC KUNENGE AFANYA ZIARA HOSPITALI YA WILAYA MSOGA

Image
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge hii leo ameanya ziara maalumu katika hospital ya Msoga kwa lengo la kukagua na kuona maendeleo ya Jengo la dhararu la (EMD) Iliyopo katika hospital ya Msoga . Akiwa katika hospitali hiyo Mhe Kunenge alipata kuona maendelea ujenzi wa jengo la hilo la dharura ambalo ujenzi huo umekamilia kwa asimilia kubwa na kilichobaki ni umalizaji wa uwekezaji wa samani,Ujenzi wa majengo mbalimbali katika hospitali hiyo Pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa uwanja wa kisasa wa Mpira wa miguu. Katika ziara hiyo Mhe Kunenge alipata wasaa wa kusalimiana na kuzungumza na wananchi waliofika katika hospitali ya Msoga kupata huduma ambapo alisema alitembelea hospitali hiyo kuona maendeleo ya ujenzi lakini pia kuona namna huduma  zinazotolewa hospitalini hapo. ''Nimekuja kuona Maendeleo ya ujenzi wa jengo ya huduma za dharura lakini pia kuona jinsi utoaji wa huduma unavyoendelea na naamini ninyi ndiyo mtawaambia huduma ina ubora ama sivyo”.Amesema Mhe.Kuneng...

HALMASHAURI YA GEITA MJI YAFANYA ZIARA CHALINZE DC

Image
     Madiwani kutoka Geita Mji wakikagua uzalisshaji wa madini ya ujenzi katika            Halmashauri ya Chalinze  Halmashauri ya Geita mji hii leo imefanya ziara katika Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani kwa lengo la kutembelea na kujifunza namna bora ya uzalishaji na utekelezaji wa madini ujenzi. Ugeni huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mh. Cornel Magembe Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Costantine Mtani ,Mkurugenzi Mtendaji Bi.Zahara Michuzi,Waheshimiwa madiwani,Wataalamu na Baadhi ya wananchi wakiwa wawakilishi wa Wananchi wenzao. Kwa niaba ya  Halmashauri ya Geita MJI,Mkuu wa Wilaya huyo Pamoja na Mwenyekiti  wameshukuru Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa Mapokezi mazuri lakini pia kwa kuwapa maelekezo mazuri ya namna bora ya uzalishaji wa miradi. ''Tunawashukuru sana kwa mapokezi mazuri sana pamoja na namna mlivyotupa maelekezo mazuri kwani hamkutuficha kitu lakini pia huu ni mwanzo tutaendelea kujifunz...

BARAZA LA MADIWANI CHALINZE LAPITISHA RASIMU YA BAJETI YA BILIONI 52.6 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Image
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze limepitisha rasimu ya bajeti  ya mwaka wa fedha 2023/2024 sh. Biln 52.6  itakayotekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.  Akiwasilisha makadirio hayo katika kikao cha Baraza la Bajeti Mkurugenzi Ramadhani Possi amesema kati ya fedha hizo sh. Biln 32.7 ni ruzuku kutoka Serikali kuu, Biln 14.9 Makusanyo ya ndani na sh.Biln 4.9 ni kutoka kwa wahisani. Amesema feha hizo zitatumika kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, mishahara ya watumishi na matumizi ya ofisi. Akizungu mza katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassan Mwinyikondo pamoja na baadhi ya Madiwani wa waamepongeza bajeti hiyo na kuasema inakwenda kuwakomboa wananchi wa Chalinze. Mwinyikondo amesema Maendeleo katika Halmashauri hiyo yanaenda kwa kasi kutokana na ushirikiano kati ya Madiwani na wataalamu. " Katika makusanyo ya ndani kwa  mwaka wa fedha 2022/2023 tulikadiria sh Biln 13 na hadi sasa tumekusanya kwa asilimia 55 kwa bajeti hii inayoend...

TAASISI YA BLUE CARBON UAE NA SERIKALI YA TANZANIA WAMETIA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO

Image
 Taasisi ya Blue Carbon UAE na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wametia saini Mkataba wa Makubaliano kuanza kwa ushirikiano wenye lengo la kukuza usimamizi endelevu wa misitu na kupunguza ukame.   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe, Dkt. Selemani Jafo amesema biashara ya kaboni itasaidia kuleta fursa nyingi hapa nchini na kusaidia kuhifadhi mazingira. Amesema hayo mara baada ya hafla ya kusainiwa kwa hati ya makubaliano ya uhusiano kati ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Kampuni ya Blue Carbon kutoka Dubai. Hafla hiyo imeshuhudiwa na Mwanamfalme wa Dubai ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon Mhe. Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum na Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana. Dkt. Jafo amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa makubaliano hayo baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha uandaaji wa kanuni na mwongozo wa biashara ya kabin...

CHALINZE DC FC YAANZA MAANDALIZI YA SHIMISEMITA 2023

Image
Timu ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeanza kujiandaa na mashindano ya SHIMISEMITA kwa kucheza mechi mbalimbali za kirafiki ikiwemo mechi ya leo ambapo timu ya Chalinze Dc imepoteza kwa magoli  8-4  dhidi ya Azam Veterani katika uwanja wa Azam Compex,Chamanzi. Akizungumza mara baada ya mchezo wa kirafiki Mbaraka Shabani (Cantona)ambaye ni Mwenyekiti wa Timu ya Azam Veterani amesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa Chalinze DC FC kwani mpaka hivi sasa pande mbili hizo zimekuwa kama ndugu. " Nimefurahishwa na ugeni wenu kwani sasa tumekuwa kama ndugu naamini mmejifunza mengi lakini pia hata sisi tumejifunza mengi sana kwani mpira mnaujua  na najua hamkutarajia kutowakuta veterani wenyewe hii ni kutokana na Timu yetu ya Azam Fc kusafiri kwenda Dodoma na viongozi ambao ndio wachezaji wetu hivyo basi niwakaribishe tena siku nyingine kwani mechi hizi za kirafiki zinatuandaa vyema kiafya na hata kimichezo".Amesema Ndg.Mbaraka Shabani. Aidha uongozi wa Klabu...