Posts

Showing posts from April, 2023

HALMASHAURI 95 ZAPATA MAGARI KUPITIA PROGRAMU YA EP4R

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),    Mhe. Angellah Kairuki amekabidhi magari 25 ikiwa ni sehemu ya Magari 200 yaliyoagizwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kwa ajili ya Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri zote nchini. Pia ameahidi kujenga bweni la wanafunzi wa kiume wa shule ya sekondari Kibasila ikiwa ni ahadi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan. Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika hafla ya ugawaji wa magari hayo Mhe. Kairuki  aliwataka Wakala wa Ununuzi Serikalini (GPSA) kukakamilisha upatikanaji wa magari mengine 105 yaliyosalia kwa ajili ya mafisa elimu hao. "Katika Halmashauri 184 zinazotakiwa kupata magari, Halmashauri 51 tayari zimepata katika awamu ya kwanza, awamu ya pili 19 na hii awamu ya tatu    magari 25 hivyo bado magari 105 kwa maofisa hayo," alisema. Aidha, ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha elimu na maslahi ya walimu nchini hivyo aliwataka maofisa hao wa...

DC-OKASH,KAMATI YA USALAMA WAFANYA ZIARA VIWANDANI CHALINZE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Halima Okash pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama amefanya ziara katika maeneo ya uwekezaji na Viwanda vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani Pwani kwa lengo la kuona Mafanikio,uendeshaji na Changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili kuweza kuzitatua ili kuweka mazingira salama kwa wawekezaji. Akizungumza katika Ziara hiyo Mhe.Okash amewapongeza wawekezaji hao kwa Uwekezaji Mkubwa wanoufanya katika Halmashauri ya Chalinze kwani ni manufaa kwa Halmashauri,Wilaya,Mkoa na hata Taifa kwa ujumla pamoja na jamii inayowazunguka pamoja na kuwaahidi kuzifanyia kazi changamoto wanazokumbana nazo ili kuendelea kuwawekea Mazingira rafiki katika Uwekezaji . “Niwapongeze wawekezaji hasa kwa uwekezaji Mkubwa mnaoufanya kwani haya ni maendeleo makubwa kwa Taifa kwani Tanzania sasa tunaouwezo mkubwa wa kutumia bidhaa za ndani na kuzisafirisha mpaka nje ya nchi na niwaahidi sisi kama Serikali tutazifanyia kazi Changamoto zote ili muwe na Mazingira rafik...